HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA
VIWAWA ilianzishwa mwaka 1924 mji wa
Brussel nchini Ubelgiji na Kadinali Joseph Cardjin nakupitishwa rasmi kama
Chama cha Kitume cha Vijana Kimataifa na Baraza la Kipapa Vatcan mwaka
1950.Kadinali Joseph Cardjin pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA na YCS alianzisha
yeye.
Makao Makuu ya
Viwawa Duniani Yako Roma – Italia.
Viwawa
iliingia Tanzania mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi, Jimbo Kuu la Dar es
Salaam, chini ya Mwanzilishi Pd. Lucas Gaemperle OFM, badaye mwaka 1960 alifika
nchini kwetu Pd. Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Pd Mansuetus ambaye
alimsaidia kwa karibu sana, padri Lucas kuueneza utume wa viwawa nchini kwetu,
na kufuatiwa na Parokia ya St. Joseph, Kurasini,Magomeni,Chang’ombe, Kibaha.
Mwanzilishi
wa viwawa duniani Kardinali Joseph Cardijn alitembelea Tanzania, jimbo la Dar
es salaam tarehe 17 – 6 – 1960.
Padri Lucas Gaemperle OFM ambaye
alikuwa mwanzilishi wake alitembea sehemu nyingi za Afrika na Ulaya kwa lengo
la kujifunza utume huu. Mwaka 1961 VIWAWA Tanzania walitembelewa na mjumbe
kutoka Makao Makuu Roma Italia na alitembelea matawi ya Dar es Salaam na Moshi.
Mjumbe huyo alifanyakazi ya kuunganisha utume huu hapa Tanzania na huko Zambia.
Mwezi Novemba 1964 Kamati kuu ya VIWAWA ulimwenguni walifanya mkutano hapa
Tanzania, Mkutano huu ulifuatiwa na ziara za mafunzo ili kuona maendeleo ya
Viwawa hapa Tanzania.
Mnamo
mwaka 1966 Viwawa walifanya mkutano mkuu wa kitaifa na ni majimbo mawili tu
ndiyo yalihudhuria Dar es Salaam na Moshi yakiwakilishwa na wajumbe kumi na
mmoja. Mwaka 1973 mkutano mkuu ulifanyika jimboni Iringa na ndipo kwa mara ya
kwanza katiba ya Viwawa iliundwa, na kupitishwa rasmi kama chama cha kitume cha
vijana na Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) mwaka 1979. Mshauri wa
kwanza wa viwawa Taifa Padri Pius Shayo aliyeteuliwa katika mkutano mkuu wa
baraza la maaskofu Tanzania uliofanyika tarehe 23 – 27 October, 1979.
Baada ya kupitishwa hapo kilitambulika
pote Tanzania kama Chama cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi Tanzania
(VIWAWA)Mpaka sasa, chama hiki kipo majimboni, kuanzia ngazi ya Jumuiya, Mtaa,
Kanda, Kigango, Parokia, Jimbo, Taifa na Kimataifa.
MAANA YA VIWAWA
VIWAWA ni chama cha kitume cha Vijana Wakatoliki
Wafanyakazi ambao wanatumwa na Kanisa ili kueneza habari njema ya kwamba Yesu
Kristu ndiye njia ya ukweli na uzima kwa vijana wote katika maisha yao ya kila siku.
Wafanyakazi: Ni vijana wa wanaume na wanawake waishio
mijini, vijijini na walio kwenye masomo, mafunzo ya fani mbalimbali, walio
katika ajira rasmi na zisizo rasmi.
Viwawa ni chama ambacho kinawaunganisha vijana na
kuwasaidia waone hali yao, kuamua juu yake katika mwanga wa Injili na
kuwaongoza kufanya matendo ya
kubadilisha hali zao na kutengeneza ziwe nzuri zaidi kwa njia ya Tafakari ya
Maisha. Chama hiki huongozwa na vijana wenyewe katika ngazi zote na huwa na
Mshauri na Mlezi kwa ngazi ya Parokia,Jimbo na
Taifa.
DIRA YA VIWAWA
Kumwona Kijana Mkatoliki Mfanyakazi anayejimudu
katika maisha yake ya kimwili na kiroho kwa kutumia njia ya Tafakari
ya Maisha.
UTUME WA VIWAWA
Kumwezesha kijana kuwa Mkristo wa kweli ambaye ana ujasiri wa kurekibisha, kuendeleza na kudumisha taratibu za utamaduni, uchumi, siasa na utaalamu kufuatana na mpango wa Mungu.
UTUME WA VIWAWA
Kumwezesha kijana kuwa Mkristo wa kweli ambaye ana ujasiri wa kurekibisha, kuendeleza na kudumisha taratibu za utamaduni, uchumi, siasa na utaalamu kufuatana na mpango wa Mungu.
MALENGO YA VIWAWA
Kuwawezesha Vijana kutambua wajibu wao katika
kujielimisha na kujitegemea katika maisha yao.
Kustawisha na kusaidia Kanisa kwa kushiriki katika kazi
za Kanisa, kuhusu maendeleo ya Kiroho, Kimwili, Kiakili na Kijamii.
Kutangaza habari za Kanisa na kujaribu kwa kila hali
kuleta uhusiano mwema baina ya vyama vya kitume,madhehebu mbalimbali na dini nyingine.
Kuchukua hatua za kufaa kuendeleza mambo yote
yanayoonekana kwamba ni ya manufaa kwa Kanisa na Ustawi wa jamii.
Kuwajenga vijana katika mazingira ya kuwa na mwenendo
mwema kwa kanuni ya Tafakari ya Maisha inayoongozwa na mtindo wa Kuona-Kuamua na
Kutenda. Na mitindo mingine ya malezi inayofaa.
Kuwakumbusha vijana wote kwamba sote tunategemeana kwa kushauriana, kuongozana na kufundishana kimwili na kiroho.
Kuwakumbusha vijana wote kwamba sote tunategemeana kwa kushauriana, kuongozana na kufundishana kimwili na kiroho.
Comments
Post a Comment